Heri ya Kuzaliwa Kwangu

 

 Heri ya Kuzaliwa Kwangu  

Siku (29 Desemba) imefika tena kwangu kujitakia siku njema ya kuzaliwa. Kwa hivyo, ninajitakia mafanikio na furaha isiyo na kikomo hasa ninapoadhimisha siku ya kuzaliwa.

Kuanzia sasa na hata milele nitamshukuru Bwana kwa kunijalia siku nyingine ya pekee hapa duniani. Katika siku hii, ninaomba iwe siku njema ya kuzaliwa na neema katika maisha yangu ya kila siku. Ninapokumbuka siku ya kuzaliwa kwangu, maneno ya Mzaburi yanapata maana kwamba: "Ni neno jema kumshukuru Bwana na kuliimbia jina lako Ee uliye juu kuzitangaza rehema zako asubuhi na uwaminifu wako wakati wa usiku" (Zab 92:1-2). Awali ya yote, nipende kutumia fursa hii kumshukuru Mungu, Baba wa mbinguni na nchi kwa kunifanya moja kati ya viumbe alivyoviumba chini ya jua, ni kwa upendo na neema yake tu kuwepo kwangu hadi leo hii kwani sina haki kuliko wale wote waliotangulia mbele ya haki; wapumzike kwa amani. Ahsante Mungu kwa baraka na neema zako ambazo zimeandamana nami tangu kuumbwa kwangu hadi leo hii ninapokushukuru kwa zawadi ya maisha. 

 Nawashukuru Wazazi, ndugu, jamaa, marafiki na watu wenye mapenzi mema

Maandiko Matakatifu yanaweka wazi kuwa, “Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako” (Kut 20:12). Nawashukuru wazazi wangu, walezi, walimu, ndugu, marafiki na watu wote wenye mapenzi mema ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa sehemu ya Maisha yangu. Ahsanteni sana Mungu awabariki nyote.

 Nawashukuru Baba Askofu, Mapadre na walezi wangu

Ni ukweli usiopingika kuwa leo ninasherehekea siku ya kuzaliwa, hii ni kwa sababu nimejaliwa mwaka wa ziada katika ulimwengu huu. Ni muda wa kuendelea kujitafakari na kuuchuchumalia utakatifu. Ninaomba na kusali kwa ajili ya maendeleo yangu ya kiroho, kichungaji, kitaaluma na kiutu ili yawe ya kufaa kwa Kanisa na jamii kwa ujumla. Ni katika hili, naendelea kujitakia siku ya kuzaliwa yenye furaha, amani, upendo na uchaji wa Mungu.

Ahsanteni wote kwa kuendelea kuwa sehemu ya maisha yangu.

Pd. Emmanuel Kimambo Nhanwa, 
Jimbo Katoliki Shinyanga, Chuo Kikuu Navarra, Pamplona, Hispania.

OMBI
Jumuika pamoja nami kufanikisha uchapaji wa vitabu vitatu vya imani na uinjilishaji vilivyoandikwa nami, na Mungu atakubariki sana. Unaweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-Pesa kwenda namba +255754985663 (Emmanuel Kimambo Nhanwa) au bonyeza HAPA.


©2023 Ekinopia Studies