Campaign to Publish the Pastoral Book
“HAKI YA MAZISHI: Kwa Mujibu wa Sheria Mkusanyo Kanoni”
Dear friends and people of goodwill,
We are joyfully launching a campaign to publish a pastoral book titled “HAKI YA MAZISHI: Kwa Mujibu wa Sheria Mkusanyo Kanoni”. This essential work seeks to unveil who has and who has no right to be buried in the Church, while also offering pastoral solutions rooted in faith, compassion, and Church teaching. It is a valuable guide for pastors, catechists, and all believers who desire clarity and wisdom in handling delicate matters surrounding Christian funeral and burial.
The total cost of publication amounts to 3,215 euros, covering editing, printing, and distribution so that this enlightening book may reach parishes, seminaries, and Christian communities everywhere. We humbly invite each of you—individuals, families, and institutions—to support this noble cause. No donation is too small; every offering, given from the heart, contributes to spreading understanding and unity within the Body of Christ.
As the Book of Tobit reminds us:
“Give in proportion to what you own. If you have great wealth, give alms out of your abundance; if you have but little, do not be afraid to give alms even of that little. ” (Tobit 4:8).
Let us respond to this divine call with generosity and faith. Your contribution will help bring “HAKI YA MAZISHI: Kwa Mujibu wa Sheria Mkusanyo Kanoni” to life—a book that will serve as a beacon of truth, compassion, and pastoral guidance in our Church today.
To donate or learn more, please contact:
- M-Pesa: +255 754 985 663
- Tigo Pesa: +255 714 384 849
- Airtel Money: +255 780 893 133
- Bizzum: +34 602 68 48 76
- PayPal: Click Here!
“A small act of love can illuminate a great many hearts"
Fr. Emmanuel Robert Kimambo
IN SWAHILI
Kampeni ya Kuchapisha Kitabu
“HAKI YA MAZISHI: Kwa Mujibu wa Sheria Mkusanyo Kanoni”
Wapendwa marafiki na watu wenye mapenzi mema,
Tunafurahia kuanzisha kampeni ya kuchapisha kitabu cha Kichungaji chenye anwani: “HAKI YA MAZISHI: Kwa Mujibu wa Sheria Mkusanyo Kanoni”. Kitabu hiki ni cha muhimu na kinakusudia kufafanua nani ana haki na nani hana haki ya kupata maziko ya kikanisa, pamoja na kutoa suluhisho la kichungaji kwa mujibu wa Sheria Mkusanyo Kanoni na mafundisho ya Kanisa. Ni mwongozo wa thamani kwa wachungaji (Maklero), walimu wa dini (Makatekisita) na waumini wote wanaopenda kujitajirisha kwa maarifa na hekima katika masuala nyeti yanayohusu mazishi ya Kikristo (Kanisa Katoliki).
Gharama ya jumla ya kuchapisha wa kitabu hiki ni euro 3,215, ikijumuisha uhariri, uchapishaji, na usambazaji ili kitabu hiki cha mwangaza kifikie makanisa, seminari, na jamii za Kikristo kila mahali. Tunawaalika kwa unyenyekevu kila mmoja wenu—watu binafsi, familia, na taasisi—kuunga mkono juhudi hii ya heshima. Hakuna mchango mdogo sana; kila sehemu, ikitolewa kwa moyo, inachangia kueneza uelewa na umoja ndani ya Mwili wa Kristo, yaani Kanisa.
Kama kitabu cha Tobiti kinavyotufundisha:
“Ukiwa na wingi utoe sawasawa na wingi wako; ukiwa na kidogo tu usiogope kutoa sawasawa na kidogo hicho” (Tobiti 8:4).
Tukumbatie wito huu wa kimungu kwa ukarimu na imani. Mchango wako utasaidia kuleta “HAKI YA MAZISHI: Kwa Mujibu wa Sheria Mkusanyo Kanoni” kuwa hai—kitabu kitakachokuwa taa ya ukweli, huruma, na mwongozo wa kichungaji ndani ya Kanisa letu leo.
Kwa kuchangia au kupata maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
- M-Pesa: +255 754 985 663
- Tigo Pesa: +255 714 384 849
- Airtel Money: +255 780 893 133
- Bizzum: +34 602 68 48 76
- PayPal: Click Here!
“Kitendo kidogo cha upendo kinaweza kuangaza mioyo mingi.”
Pd. Emmanuel Robert Kimambo